KLABU YA HAKI ZA BINADAMU SHULE YA SEKONDARI MWANDIGA KUWAJENGEA UWEZO WANAFUNZI WENZAO
16 Feb, 2025

Ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora THBUB ukiongozwa na Kamishna Mhe. Amina Talib Ali umezindua klabu ya haki za binadamu Shule ya Sekondari ya Mwandiga iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma DC leo 13 Februari 2025.
Uzinduzi wa klabu hiyo umefanyika wakati Ujumbe huo ulipofika Shuleni hapo kwa lengo la kutoa elimu ya kusimamia na kulinda
haki za binadamu na uelewa wa Misingi ya Utawala Bora na kuitaka klabu hiyo kuwa balozi wa kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi wenzao.
Aidha Ujumbe wa THBUB umetoa elimu kwa Wanafunzi hao namna ya kupinga na kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa vikitokea katika jamii mbalimbali