MASUALA YA BAHARINI NI JICHO LA HAKI ZA BINADAMU

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi, Utafiti na Nyaraka, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi.Jovina Muchunguzi amesema kuwa masuala ya bahari ni masuala ya haki za binadamu na kuwa jicho la haki za binadamu katika usimamizi wa bahari ni jambo muhimu.
Bi Muchunguzi hayo wakati akiwasilisha mada iliyohusu “muungano wa kimkakati na nafasi ya Taasisi za Kitaifa za Haki za Binadamu (NHRIs) katika usimamizi wa bahari-uzoefu kutoka Afrika na Amerika ya Kusini. Mada hiyo ilitolewa tarehe 10 Juni, 2025 katika kikao cha pembezoni kando ya Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari (UNOC3) unafanyika Jijini Nice nchini Ufaransa kuanzia tarehe 9-13 Juni, 2025.
Bi. Muchunguzi alisema kuwa THBUB katika kutekeleza majukumu yake ya kikatiba ya kukuza, kulinda na kuhifadhi haki za binadamu nchini inaangalia haki za wavuvi wadogo kupitia mipango mbalimbali, ikiwemo kufanya tathmini ya awali ya hali ya haki za wavuvi wadogo wadogo katika upatikani na usimamizi na matumizi ya Rasilimali za Bahali.
“ Matokeo ya awali ya kazi hii yameakisi umuhimu wa ushirikishwaji wa wavuvi na jamii ya wavuvi wadogo wadogo, hali isiyo ya kuridhisha ya miundo mbinu ya uvuvi, migogoro ya ardhi maeneo ya kutua samaki, mabadiliko ya tabia nchi, ugumu wa ufikiaji rasilimali za bahali; uvuvi haramu; uharibifu wa mazingira, mazingira mabovu ya kazi”.alisema Bi.Muchunguzi
Ameongeza kuwa THBUB imewajengea uwezo watumishi kuhusu utekelezaji wa haki za wavuvi wadogo kwa kimarisha uwezo wao katika kufanya chunguzi, mapitio ya sheria, utafiti na elemu kwa umma.
Aidha,Bi Muchunguzi amebainisha kuwa zipo juhudi za serikali kupitia kutengeneza Mpango kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na Biashara unaopendekeza kuimarisha haki za wavuvi wadogowadogo kupitia usimamizi wa maingira na rasilimali za Bahari, uwepo wa mipango ya usimamizi wa Bahari kama “marine spatial plans”.
“Kazi huu ambao umesimamiwa kutengenezwa na THBUB unaleta matumaini katika kuhakikisha Haki za ardhi, rasilimali asilia, utamaduni, maji, chakula, mazingira safi na salama, pamoja na haki za kazi na usalama kazini zinapewa kipaumbele katika Uchumi wa bluu”.alisema Bi. Muchunguzi