ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Mkutano wa Kujadili taarifa ya Itifaki ya Maputo(Maputo Protocal) iliyoandaliwa na PATHFINDER Kushirikiana na TAWLA

08 Sep, 2022
Mkutano wa Kujadili taarifa ya Itifaki ya  Maputo(Maputo Protocal) iliyoandaliwa na PATHFINDER  Kushirikiana na TAWLA

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe.Dkt Thomas Masanja amelipongeza Shirika lisilo la Kiserikali Pathfinder na TAWLA kwakuandaa taarifa ya utafiti  kuhusu  Ibara za Itifaki ya Maputo(Maputo Protocal) iliyojadiliwa  Agosti 31,2022 katika Ukumbi wa Nashera Hotel  ulipo Jijini Dodoma.

Mhe. Masanja alitoa pongezi hizo wakati  wakufunga  kikao cha kujadili taarifa hiyo iliyo  wasilishwa na Dr. Kalekwa Mtaalamu kutoka Shule ya Sheria(LAW SCHOOL).

Aidha Mhe.Dkt Masanja  alitoa rai kwa wadau hao kushirikisha wadau wengi wanahusika na masuala ya haki za wanawake ili  kufikia lengo la utafiti huo.

“Niwapongeze kwa majadiliano mazuri,ni muda muwafaka sasa wakushirikisha  wadau wengine   kuongeza wigo wakupokea mawazo tofauti kuhusu haki za wanawake”Alisema Mhe. Dkt Masanja

Kwa upande wake Bw.Meshack Mollel  Meneja mradi  Pathfinder aliwashukuru wajumbe kwakuhudhuria kikao hicho na kutoa mawazo yao kupitia taarifa iliyowasilishwa na kuahidi kufanyia kazi michango yote iliyotolewa na wajumbe wa kikao hicho.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Wakurugenzi  kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Maafisa wengine wa Tume, Meneja Mradi na Afisa Mradi kutoka Pathfinder, na Mratibu kutoka TAWLA.