ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

*MWAIMU AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA BALOZI WA USA NCHINI* 

07 Sep, 2023
*MWAIMU AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA BALOZI WA USA NCHINI* 

 

Leo Septemba 7, 2023 Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Mathew Mwaimu (Jaji Mstaafu) amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Balozi wa Marekani nchini Tanzania, ulipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za Tume zilizopo mtaa wa Kilimani jijini Dodoma.

Ujumbe huo wa watu watatu uliongozwa na Mshauri wa masuala ya Siasa na Uchumi katika Ubalozi huo, Bwana Jonathan Howard aliyeambatana na Bwana Andy Allen  na Bi. Beatrice.

Katika mazungumzo yao Ujumbe huo ulipata fursa ya kuifahamu zaidi Tume na majukumu yake na   Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu.

Pia, katika mazungumzo yao viongozi hao walijadili maeneo mbalimbali ya mashirikiano kwa lengo la kukuza na kulinda haki za binadamu nchini.

Mkurugenzi wa  Malalamiko na Uchunguzi, Bi. Suzana  Pascal aliambatana na Mhe. Mwenyekiti wa Tume katika mazungumzo hayo