ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Mwenyekiti wa THBUB akutana na kuzungumza na Balozi wa Sweden nchini

14 Feb, 2024
Mwenyekiti wa THBUB akutana na kuzungumza na Balozi wa Sweden nchini

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Mathew Mwaimu (Jaji Mtaafu) leo Februari 2, 2024amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Charlotta Ozaki Macias na ujumbe wake.

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Charlotta Ozaki Macias aliipongezaTume kwa jitihadakubwa inazofanya katika kulinda na kutetea haki za binadamu nchini; na pia katika kutoa ushauri kwa Serikali na wadau wengine kuhusu utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu.

Aidha, Mhe. Charlotta alipenda kujua hatua iliyofikiwa na Tumekatika kuandaaMpango Kazi wa Kitaifa wa Biashara na Haki za Binadamu na namna ilivyojipanga kuwashirikisha wafanyabiashara. 

Mhe. Charlotta Ozaki Macias aliifahamisha Tumekuwa nchi yake kupitia Ofisi yake ya ubalozi nchini Tanzania inatekelezaMpango Mkakati wake wa miaka minne (2020-2024.Mpango huo umejikita katika kuangalia maeneo ya haki za binadamu, usawa wa kijinsia,mazingira, elimu na ukuaji wa kiuchumi na mabadiliko ya tabia nchi. Hivyo, anaiona kwa THBUB kushirikiana na Sweden katika baadhi ya maeneo hayo.

Pia, Mhe. Balozi Macias alieleza kuwa nchi yake inao uzoefu mkubwakuhusuutekelezaji wa masuala ya Biashara na Haki za Binadamu, hususan uwepo wa mifumo na jinsi wanavyoshughulikia malalamiko ya kibiashara. Hivyo, alibainisha kuwa hiyo ni fursa nyingine kwa Tume katika maandalizi ya Mpango Kazi wa Kitaifa wa Biashara na Haki za Binadamu.

Katika mazungumzohayo Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Charlotta Ozaki Macias, aliambatana na Balozi wa Biashara Endelevu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Sweden, Bi. Cecilia Ekholm. Katika nyakati tofauti wawili hao walisifia uhusiano imara uliopo kati ya nchi yao na Tanzania na kuahidi kuyakuza zaidi, hususani katika katika kukuza na kulindaHaki za Binadamu nchini.

Kwa upande wake, Mhe. Jaji Mstaafu Mwaimu ameishukuru Serikali ya Sweden kwa mchango wake wa kihistoria katika uendelezaji wa masuala ya haki za binadamu nchini Tanzania.

Katika mazungumzo hayo pande hizo mbili zimekubaliana kuendelea kufanya majadiliano ya namna ya kushirikiana katika maeneo kadhaa, ikiwemo:Kutoa elimu ya uraiana ufuatialiaji wa chaguzi nchini; kufuatilia haki za watu walipo vizuizini; kuimarisha misingi ya utawala bora ili kukuza haki za binadamu; na maandalizi ya Mpango Kazi wa Kitaifa wa Biashara na Haki za Binadamu.

Ziara ya Balozi huyo wa Sweden, Mhe. Charlotta Ozaki Macias, ni ufuatiliaji wa ziara yake ya awali aliyoifanya Mei 5, 2023 ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Mwenyekiti wa THBUB na viongozi wengine wa Tume.