NAIBU WAZIRI WIZARA YA KATIBA NA SHERIA AIPONGEZA THBUB KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA WANANCHI
09 Jul, 2025

Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Jumanne Abdalah Sagini
amepongeza kazi kubwa inayofanywa na THBUB katika kuhudumia wananchi kwa kutoa elimu ya masuala ya haki za binadamu na misingi ya utawa bora, kupokea na kushughulikia malalamiko yao.
Mhe. Sagini ametoa pongezi hizo alipotembelea Banda la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Maarufu Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Maonesho vya Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo Julai 8, 2025.
Aidha ametoa wito kwa THBUB kuendeleza ushirikiano na Wizara ya Katiba na Sheria katika kutoa elimu kwa umma kuhusu Haki za binadamu, utawara bora na masuala ya Sheria kwani uelewa wa wananchi bado ni mdogo