THBUB KUSHIRIKIANA NA MAMLAKA YA KUDHIBITI DAWA ZA KULEVYA.

Katika kumlinda mtoto na kuandaa jamii bora ya sasa na baadae ipo haja ya mashirikiano baina ya Tume ya Haki za Binadamu na Mamlaka ya Kudhibiti dawa za Kulevya.
Hayo amesemaKamishna wa THBUB mhe Amina Tali Ali wakati akizungumza na Kamshna Generali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya alipotembelea banda la THBUB katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara "Sabasaba"Jijini Dar es Salaam Julai 5,2025
Mhe.Amina amesema kuwa watoto wengi wa sasa uingia katika makundi mabaya na kujihusisha na kutumia dawa za kulevya ,ambapo upelekea kupoteza haki zao za msingi.
"Kushirikiana kwa THBUB na DCEA itasaidia katika kuleta watoto hawa katika mstari"amesema mhe. Amina
Kwa upande wake Kamishna Generali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Bw.Aretas Lyimo amesema kuwa ushirikiano utasaidia kupunguza au kupoteza kabisa matumizi ya dawa za kulevya kwakuwa watoto watakua wamepata elimu ya haki za binadamu ,ambayo wakitumia dawa za kulevye wanapoteza haki zao"
Bw Lyimo amebainisha haki mbalimbali ambazo mtoto anaeza kupoteza anapotumia dawa za kulevye ikiwemo haki ya kuishi,haki ya afya na elimu na nyingine "
Aidha Bw.ameomba THBUB kushirikiana kwa pamoja kupitia Klabi za haki za binadamu za ili kujenga kutoa elimu ambayo inawasaidia watoto kutambua madahara ya dawa za kulevya na kupata haki zao