ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB na Ujumbe wa EU wakutana kuzungumzia utekelezaji wa mapendekezo ya Haki Jinai

25 Jan, 2024
THBUB na Ujumbe wa EU wakutana kuzungumzia utekelezaji wa mapendekezo ya Haki Jinai

Leo Januari 24,2024 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imekutana na Ujumbe wa Umoja wa Ulaya(European Union - EU) na kufanya mazungumzo kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Rais ya Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai nchini.

 

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisi Kuu ya THBUB Kilimani jijini Dodoma, Tume iliujulisha Ujumbe huo kuwa tayari imekwisha chukua hatua kadhaa za maandalizi ya utelezaji wa mapendekezoyaliyotolewa na Kamati hiyo ya Mheshimiwa Rais, na kwamba ingefurahi kupata msaada wa wadau katika kutekeleza jukumu hilo.

 

Kwa upande wake, Ujumbe huo uliifahamisha Tume kuhusu utayari wa EU kuiwezesha Tume katika kutekeleza baadhi ya vipengele vya mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Haki Jinai.

Miongoni mwa maeneo ambavyo EU inaweza kuisaidia Tume kwa mujibu wa Ujumbe huo ni pamoja na: Uanzishaji wa Divisheni ya Haki Jinai, mafunzo kwa watumishi, kupata vitendea kazi na gharama za uendeshaji katika baadhi ya maeneo.

Mtaalamu wa masuala ya haki na utawala wa sheria, Bi.Nathalie Vandevelde aliongoza Ujumbe wa EU katika mazungumzo hayo akiambatana na Mshauri Mwelekezi, Wakili Clarence Kipobota.

Washiriki wa mazungumzo hayo yaliyoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe.Mohamed  Khamis Hamad kwa upande wa Tume walikuwa: Wahe. Makamishna Dkt. Thomas Masanja, na Mhe.Nyanda Shuli; Katibu Mtendaji wa Tume,Bwana Patience Ntwina; Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria, Bwana Nabor Assey;na Mkurugenzi Msaidizi - Utekelezaji wa Sheria, Bwana Gabriel Lubagila.