THBUB TAWI LA DAR ES SALAAM WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
09 Mar, 2025

Watumishi Wanawake wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Tawi la Dar es salaam wameungana na Wanawake wa Mkoa wa Dar es salaam kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika leo Machi 8, 2025, katika viwanja vya Leaders Club, Jijini Dar es salaam.
Mgeni Rasmi wa Maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Albert Chalamila na Kauli mbiu ikiwa ni “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwekezaji.