ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB yaandaa Kikao Kazi cha Mapitio ya Maandiko, Machapisho na Nyaraka kuhusu Utekelezaji wa Biashara na Haki za Bindamu nchini.

21 May, 2024
THBUB yaandaa Kikao Kazi cha Mapitio ya Maandiko, Machapisho na Nyaraka kuhusu Utekelezaji wa Biashara na Haki za Bindamu nchini.

Tume ya Haki za Binadamu na  Utawala Bora (THBUB) inaendelea na hatua za Uandaaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Biashara na Haki za Binadamu  utakaosaidia kuongeza uelewa wa wadau na jamii kuhusu ya Biashara na Haki za Binadamu na Mwongozo wa Kanuni za Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu kwa ujumla. Hayo amebainisha Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe.Mohamed Khamisi Hamadi, wakati akifungua Kikao Kazi cha Mapitio (Literature Review) ya Mikataba ya Kimataifa, Kikanda, Sera, Sheria, Kanuni, Miongozo, Maandiko na Machapisho mbalimbali yanayohusiana na masuala ya haki za binadamu na biashara ili kutathmini utekelezaji wake na kuandaa taarifa hali ya utekelezaji, mapungufu, na kutoa mapendekezo yatakaosaidia kuchagua maeneo ya kipaumbele vitakavyoakisi mpango kazi huo.

 

Kikao kazi hicho kiliratibiwa na THBUB na miongoni mwa washiriki ni Waheshimiwa Makamishna wa THBUB, Katibu Mtendaji Msaidizi wa THBUB, Wakurugenzi kutoka THBUB, Watumishi wa THBUB, na Wadau kutoka Wizara za Kisekta, Idara na Taasisi za Serikali, pamoja na AZAKi  kutoka Tanzania Bara na Zanzibar. Kikao hicho kimefanyika tarehe 20 Mei, 2024  katika Ukumbi wa Golden Crest Jijini Arusha.

 

Akizungumza katika hotuba yake ya ufunguzi, Mhe. Mohamed alisema kuwa Kikao Kazi hicho kinaendelea kufanya mapitio ya Nyaraka, machapisho  na maandiko mbalimbali kupitia makundi ya Kisekta “Thematic Working Groups” (TWGs) ambapo Timu ya Wataalamu imeandaa nyenzo za ukusanyaji wa taarifa hizo. Mhe.Mohamed alitoa wito kwa washiriki  kupitia vyema nyaraka hizo yanayohusu maeneo saba (7) ya vipaumbele vya kisekta vilivyoidhinishwa na Kamati Tendaji ya Kitaifa ambayo ni: Uziduaji na Nishati ,Uzalishaji na Usindikaji, Kilimo na Uchumi wa Buluu, Utalii na Ukarimu, Ujenzi na Usafirishaji, Mawasiliano ya Kidigital, na Biashara na Fedha.

 

"Kazi hii ya mapitio ya nyaraka ni muhimu sana kwaajili ya kuboresha Tathimin ya Hali ya Haki za Binadamu na Biashaara iliyofanywa na THBUB mwaka 2017" alisema Mhe. Mohamed. Aidha, Mhe. Mohamed alitoa shukrani kwa Serikali zote mbili, yaani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Taasisi na Idara Serikali na Asasi za Kiraia kwa kuhakikisha THBUB inatekeleza vyema jukumu la kuratibu Uandaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadaku na Biashara.

THBUB ilifanya tathmini ya Hali ya Haki za Binadamu na Biashara kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa Serikali kutoka pande zote za Muungano na Wadau wengine na kuendelea kushirikiana na wadau hao katika kueneza na kuhamasisha ajenda ya haki za binadamu na biashara nchini.