THBUB YAHAMASISHWA KUWA NA MALENGO YANAYO AKISI DIRA YA MAENDELEO YA 2050

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Franklin Rwezimula ameitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, (THBUB) kuwa na mchango katika kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050 ambayo imejengwa juu ya misingi ya utawala bora, utawala wa sheria na haki za binadamu.
Bw. Rwezimula ameyasema hayo leo Septemba 23, 2025 wakati akifungua kikao cha ndani “retreat” cha Tume na Menejmenti ya THBUB kilichofanyika katika hoteli ya Edema Mkoani Morogoro. Kikao hicho kimelenga kuboreshaji taswira, kuimarisha nafasi na kuongeza ufanisi wa THBUB katika kutekeleza majukumu yake.
Bw, Rwezimula amesema Serikali, inathamini mchango wa THBUB katika kuhifahi haki za binadamu na misingi ya utawala bora ambayo ndio ni miongoni mwa misingi ya Dira ya Maendeleo ya nchi ya 2050.
“Msingi Mkuu wa Dira ya 2050 ni utawala bora, amani, usalama na utulivu” Amesema Bw. Rwezamula
Bw. Rwezamula amesema dira ya 2050 inatambua kwamba Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuboresha demokrasia na utawala bora lakini bado inakabaliana na changamoto kadhaa za kiutawala.
Hivyo amewataka Makamishna pamoja na menejimenti ya THBUB kutumia kikao hicho cha ndani katika kujadiliana namna nzuri ya kuimarisha taasisi ili iwe sehemu ya kuchangia katika kutekeleza Dira ya Maendeleo ya 2050.
Akielezea kuhusu matarajio ya Serikali, Bw. Rwezamula amesema Serikali na wananchi wana matarajio makubwa kutoka kwa THBUB
Naye Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Mathew Mwaimu Jaji(Mst), akitoa shukrani kwa niaba ya THBUB ameishukuru Wizara ya Katiba na Sheria kwa mchango mkubwa inaoendelea kuutoa kwa THBUB kwa namna Wizara inavyoiangali kwa jicho la kipekee.
Mhe. Jaji ( Mst) Mwaimu amesema baada ya kikao hicho cha ndani, THBUB inatarajia kuwa na maazimio ya pamoja ya utekelezaji wa majukumu ya ili kuhakikisha THBUB mpya inazaliwa.
Aidha, Mhe. Jaji ( Mst) Mwaimu amesema THBUB ipo tayari kuendelea kushirikiana na Wizara katika nyanja zote za masuala ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya 2050.