THBUB YAKUTANA NA VIONGOZI WA CHADEMA
                            
                                 28 Aug, 2024
                            
                                
                             
                                Agosti 27, 2024, Ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ukiongozwa Mhe. Nyanda Josiah Shuli, Kamishna wa THBUB umetembelea ofisi ya Makao Makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kukutana na Mwenyekiti wake Mhe. Freeman Aikael Mbowe na Katibu mkuu Mhe. John Mnyika, jijini Dar es salaam.
Lengo la ziara hiyo ni kufanya majadiliano kuhusu tukio la ukamataji wa viongozi na wanachama wa CHADEMA Mkoani Mbeya.

