ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YATOA MAFUNZO KWA ASKARI JESHI LA POLISI KUHUSU HAKI NA WAJIBU SONGWE

22 Sep, 2025
THBUB YATOA MAFUNZO  KWA ASKARI JESHI LA POLISI KUHUSU HAKI NA WAJIBU SONGWE

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeendelea kutoa mafunzo ya Haki za binadamu na wajibu wa  Askari wa Jeshi la Polisi katika mikoa mbalimbali nchini ukiwapo Mkoa wa Songwe ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuimarisha uelewa na utekelezaji wa jukumu la  ulinzi na uhifadhi wa haki za binadamu kuelekea Uchaguzi Mkuu. 


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwa Mkoa wa Songwe, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa THBUB,  Bw. Jackson Nyamwihula amewasisitiza askari polisi kuheshimu haki za binadamu na kufuata misingi ya utawala bora, hasa katika kipindi hiki  cha uchaguzi. 

Amesema kuwa ni muhimu kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa amani na utulivu vinaendelea kudumishwa nchini kabla, wakati na baada ya uchaguzi.


Aidha, THBUB inaendesha mafunzo pia inaendesha mafunzo kama haya kwa waandishi wa habari, kwa lengo la kuhakikisha kuwa wadau wote wa uchaguzi wanakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu haki za binadamu na wajibu wao wakati wa Uchaguzi.