ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YAZINDUA CLUB YA HAKI ZA BINADAMU CHUO CHA MIPANGO DODOMA

11 Apr, 2022
THBUB YAZINDUA CLUB YA HAKI ZA BINADAMU CHUO CHA MIPANGO DODOMA

Haki za Binadamu ni jambo la mtambuka linagusa kila Nyanjakatika maisha ya binadamu.

Hayo alisema Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora(THBUB) Dkt Fatma R.Khalfan wakati wa Uzinduzi wa Klabu ya haki za binadamu na utawala bora katika Kongamano la kumbukizi ya Hayati Abeid Aman Karume,Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lililoandaliwa na Umoja wa Klabu zilizopo katikaChuo cha Mipango Aprili 7,2022.

Dkt Fatma alielezea jitahada kubwa zilizofanywa na Hayati Abeid Amani Karume katika kuleta usawa na kuinua heshima na utu wa wananchi wa Zanzibar.

Kwa upande wa kuitambulisha Tume alisema kuwa Ibara ya 129 mpaka 131 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 imeeleza majukumuya Tume,ikiwemo kuhamasisha jamii kuhusu masuala yahaki za binadamu misingi ya utawala bora,kupokea malalamiko,kufanya uchunguzi na utafiti kuhusu masuala ya haki za binadamu na utawala bora kama ikitokea uvunjifu wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora imekiukwa.Sambamba na utoaji wa mapendekezo katika sheria mbalimbali zinazosimamia maswala ya haki za binadamu.

‘Tume ina majukumu mengi hayo ni baadhi ya majukumu ambayo nimeyataja ili muweze kufahamu kwa ufupi’.Alisema Dkt Fatma

Aidha Dkt. Fatma alieleza kuwa Tume imeingia mkatabawa mashirikiano na asasi za kiraia 21 katika kusimamia maswala ya haki za binadamu.

‘Asasi hizi za kiraia zinashirikiana na Tume katikakutoa elimu ya masuala ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora’’Alisema Dkt Fatma

Kwa upande wake Bwa. James Kalulu, Mratibu wa Umoja wa Klabu hizo amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kushirikiana na kutafakari mambo mazuri yaliyofanywa na mzee wetu Hayati AbeidAmani Karume sambamba na kuhamasisha vijanakushiriki kwa dhati kwenye shuguhuli za kizalendo na kujenga Taifa bora.

Bwa.Kalulu alitoa shukrani kwaTume kwakutoa uelewa wa pamoja kuhusu Tume ya haki za binadamu na Utawala Bora pamoja na kuzindua Klabu ya haki za binadamu.

‘Awali nilikua nafikiri Tume hii ni taasisi isiyoyakiserikali kupitia maelezo ya Kamishna nimepata kuielewa vizuri zaidi,Tunashukuru’’Alisema Kalulu

Uzinduzi wa Klabu ya haki za binadamu katika Chuohikoni moja ya mikakati ya Tume kuanzisha Klabu katika zoezi la kuanzisha Klabu katika Taasisi za elimu kuanzia shule ya msingi mpaka vyuo vya elimu ya juu nchini.