THBUB YAZINDUA KLABU YA HAKI ZA BINADAMU SHULE YA SEKONDARI YA WAVULANA KIGOMA

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Mhe. Amina Talib Ali amezindua Klabu ya Haki za Binadamu katika Shule ya Sekondari ya Wavulana Kigoma, Februari 10, 2025.
Uzinduzi huo umefanyika wakati Ujumbe wa THBUB ukiongozwa na Kamishna Mhe. Amina Talib Ali ulipofika Shuleni hapo kwa lengo la kutoa elimu kuhusiana na haki za binadamu na misingi ya Utawala Bora.
Elimu hiyo ilijikita katika masuala ya haki za watoto na ukatili dhidi ya watoto na namna ya kupambana na ukatili kwa kutoa taarifa katika mamlaka husika.
Aidha, Wanafunzi hao wameishukuru THBUB kwa kufika Shuleni kwao na kuwapa elimu hiyo na kuahidi kuwa kupitia Klabu hiyo wataendelea kueneza elimu hiyo Shuleni hapo na katika jamii zao kuhusiana na masuala ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.