THBUBYAPOKEA MAlALAMIKO ZAIDI YA 2923 YA UVUNJIFU WA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA.

Miongoni mwa majukumu ambayo THBUB inayotekeleza ni kupokea Malalamiko ya Wananchi yanayohusu ukiukwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora
Hayo amesema Kamishna Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe.Amina Talib Ali wakati akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea banda la THBUB katika Maonesho ya Kitaifa ya Biashara Julai 4,2025 Jijini Dar es Salaam.
Mhe.Amina amesema kuwa malalamiko ya uvunjifu wa haki za binadamu bado yapo na katika kipindi cha miaka minne jumla ya malalamiko 2923 yamepokelewa na THBUB ambayo tunaendelea kuyashughulikia
"Malalamiko hayo sio lazima alalamikiwe kiongozi hata mtumishi ambaye amepewa jukumu lakutekeleza asipofanya hivyo anakiuka misingi ya utawala bora” mesema mhe.amina
Pia.Mhe.Amina ametaja malalmiko yalilopokelewa zaidi katika kipindi hicho ni kuhusu ardhi na mifuko ya hifadhi ya Jamii
"THBUB tunapokea malalamiko mengi ya wastaafu kupata kiinua mgongo ambacho hakutarajia au kutopata haki kwa wakati ,changamoto hii inatokana taasisi aliokua anafanyia kazi haifikishi michango kwa wakati lakini THBUB inasaidia mtu huyo apate haki yake "amesema mhe.Amina
Mhe.Amina ametaja changamoto mbalimbali ya ushughulikiaji wa malalamiko hayo ikiwemo kwa baadhi ya Taasisi zinzolalamikiwa kutokuwa na ushirikiano pindi THBUB inapopeleka taarifa ya kulalamikiwa
"THBUB inapokea na kupeleka kuwasilisha malalamiko kwa mlalamikiwa ,THBUB inaandika barua lakin hayajibiwi kwa wakati na kuna muda haijibiwi kabisa "
Nitoe wito kwa viongozi wa taasisi tunapowandikia barua,watujibu kwa wakati ili tuweze kuwajibu walalamikaji kwa wakati ili wapate haki zao