TIMU YA HAKI WANAWAKE KAMBA YAENDELEA KUFANYA VIZURI - MASHINDANO YA SHIMIWI.

Timu ya Wanawake Haki Kamba imeendelea kufanya vizuri katika mashindano ya SHIMIWI Jijini Mwanza.
Akizungumza mara baada ya mchezo kati ya timu hiyo na Uchukuzi mapema leo Septemba 4, 2025 kwenye Uwanja wa Furahisha, Nahodha wa Haki Wanawake Kamba Bi. Pili Juma alieleza kuwa, kuendelea kufanya vizuri kwa Timu hiyo kutokana na wachezaji kuwa na ushirikiano, nidhamu pamoja na kuzingatia mazoezi. "Kufanya vizuri kwa Timu ya Wanawake kunatokana na wachezaji kuwa na ushirikiano, nidhamu pamoja na kuzingatia mazoezi." Alisema Bi. Pili.
Timu ya Haki Kamba Wanawake inatarajia kucheza mchezo wa kukamilisha hatua za Makundi na Timu ya Madini Septemba 5, 2025, wakati Timu ya Kamba Wanaume imefuzu hatua ya Makundi na inatarajia kukutana na timu ya Ikulu mapema Jumatatu Septemba 08, 2025.