ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA  UTAWALA BORA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KIGOMA

11 Feb, 2025
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA  UTAWALA BORA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KIGOMA

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora Mhe.Bi Amina Ali amesema Tume inatarajia kutoa elimu kuhusu misingi ya haki na Utawala bora kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kigoma kwa lengo la kuwawezesha Wananchi kutambua haki zao na kudumisha Utawala unaozingatia haki za binadamu.

Kamishna Mhe.Amina ametoa kauli hiyo leo tarehe 10 Februari 2025 wakati akizungumza na Waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kuhusu zoezi la kutoa elimu kwa wananchi katika Halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Kigoma.

Amesema Tume itatoa elimu kwa watendaji wa Wilaya lakini pia kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara na kwamba watatumia mikutano hiyo kuitambulisha Tume pamoja na kuwasikiliza wananchi na kupokea malalamiko yanayohusu Haki za Binadamu na Utawala bora kwenye maeneo yao.
"Tutakua tunazungumza pamoja sisi na Wananchi,sisi tutatoa elimu waielewe lakini pia na wao waelewe haki zao na misingi ya Utawala bora,pale ambapo imetokea kasoro ama imekiukwa basi waweze kujua na waelewe kwamba Tume tunapokea malalamiko" amesisitiza Mhe.Amina 

"Baada ya kupokea malalamiko tunayafanyia uchunguzi wa kina kuweza kujua lalamiko,nani aliyefanya na ni nini kilichotokea na baadaye tunatoa mapendekezo yetu kwa Serikali"

Aidha Mhe.Amina amesema elimu ya misingi ya Haki za Binadamu na Utawala bora itatolewa pia kwa Wanafunzi kwenye shule na vyuo mbalimbali,ili kuwajengea uelewa Wanafunzi kwaajili ya mustakabali wa kuwa na viongozi bora siku za usoni.