ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

*WADAU WAKUTANA KUJADILI ITIFAKI YA MAPUTO*

23 Aug, 2023
*WADAU WAKUTANA KUJADILI ITIFAKI YA MAPUTO*

 

Leo Agosti 21, 2023 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, kwa kushirikiana na  PATHFINDER na TAWLA wamewaleta pamoja wadau mbalimbali wa kutoka Mashirika yasiyo ya Kiserikali kujadili masuala yaliyobainika baada ya mapitio ya Itifaki ya Maputo.

Lengo la majadiliano hayo ya siku moja yaliyofanyika Holiday Inn hotel lilikuwa kukusanya maoni na mapendekezo ya wadau hao kwa ajili ya kuishauri Serikali.

Miongoni mwa Washiriki wa kikao hicho walikuwa ni Wajumbe kutoka TAMWA, TAWLA, LHRC, Msichana Initiative, TANLAP, AGOTA, na Engender Health.

Wengine ni kutoka UMATI, WGNRR, MST, Young and Alive Initiative, MDM, Haki Elimu, WPC-ULINGO na Pathfinder International.