WANANCHI WANA HAKI YA KUPATA TAARIFA KIPINDI CHA UCHAGUZI

Wakazi wa Tanga wameelezwa kuwa pamoja na kuwa na haki ya kuchagua viongozi wao, uhuru wa kukusanyika na kutobabaguliwa, wanayo haki ya kupata taarifa kuhusu masuala ya uchaguzi.
Hayo yameelezwa na Afisa Uchunguzi Mkuu kutoka Ofisi ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bi. Nancy Ngula kupitia kipindi cha redio Nuur Mkoani Tanga Septemba 22, 2025.
Haki ya kupata taaarifa inawawezesha watanzania wenye sifa kupata taarifa kuhusu sheria, taratibu na miongozo ya uchaguzi ambazo zitawawezesha kufanya maamuzi sahihi.
Naye Afisa Mchunguzi Mkuu, Bw. Lazaro Mawingo, akiitambulisha THBUB na majukumu yake, amesema kuwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ni taasisi huru ya Muungano ambayo inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Majukumu hayo ni pamoja na kuhamasisha nchini hifadhi ya haki za binadamu na wajibu wa jamii, kupokea malalamiko na kuyashughulika, kufanya uchunguzi na utafiti wa masuala ya haki za binadamu.
Katika kipindi hicho cha redio, wananchi pia wamekumbushwa kutunza amani ya nchi katika kipindi chote cha uchaguzi ili kutoa fursa kwa watanzania wenye sifa kushiriki mikutano ya hadhara na kupiga kura siku ya tarehe 29 Septemba, 2025.
THBUB inashiriki vipindi vya redio na television nchini ili kutoa elimu ya haki na wajibu kwa jamii katika kipindi cha uchaguzi.