WANDISHI WA HABARI TUMIENI KALAMU ZENU VIZURI KUDUMISHA MSHIKAMANO NA AMANI- THBUB

Tume huru ya haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB )imewataka waandishi wa habari mkoani Tabora kufuata miiko na kanuni za uandishi wa habari kwa kuzingatia usawa, kuepuka matumizi mabaya ya lugha ili kudumisha mshikamano na amani hususani kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29,2025.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi msaidizi elimu kwa Umma na Mawasiliano kutoka THBUB , Zawadi Msalla ,wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Tabora juu namna bora ya kutoa taarifa zao .
"Waandishi wa habari tumieni kalamu zenu vizuri ili kuijenga Tanzania yenye mshikamano ,ili kuweza hata kufanya Tanzania iwe kati ya nchi zinazohesabika kama kisiwa cha amani" Zawadi alisema .
Bi. Zawadi , ameongezea kuwa waandishi wa habari wanayo nguvu kubwa kuijenga nchi yenye mshikamano na amani kupitia taarifa wanazo toa hivyo hawana budi kuzingatia misingi na weledi katika kazi zao.
Kwa upande wao, baadhi ya waandishi wa habari akiwemo Lubango Mleka , Maiko George na Said Kapalila , wamesema mafunzo hayo yamewaimalisha katika namna bora ya kuripoti kwa weledi na kwa kuzingatia misingi ya uandishi wa habari hususani kuelekea uchaguzi mkuu