WATUMISHI AJIRA MPYA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA (THBUB) WAAPISHWA

eo Januari 16, 2025 Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ( THBUB) Mhe. Mathew P. M Mwaimu (Jaji Mstaafu) amewapisha jumla ya watumishi wapya watano (5) ambao ni Maafisa Uchunguzi watatu (3) na Maafisa Sheria wawili (2).
Uapisho huo umefanyika katika Ofisi za Mwenyekiti wa THBUB zilizopo Makao Makuu Dodoma na kushuhudiwa na Afisa Rasilimali watu Bi. Irene Fisima na Afisa Uchunguzi Mkuu Bw. Fadhili Muganyizi.
Katika uapisho huo Mhe. Mwaimu amewataka Watumishi wa THBUB kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia Sheria na Taratibu za Utumishi wa Umma.
"THBUB ipo kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa aina zote, wapo wanaofahamu vyema Sheria na Haki zao na pia wapo wale wanaozifahamu kwa kiasi lakini wanahitaji haki ya kile wanachoamini. Hivyo, niwaombe pia ninyi mlioajiriwa sasa na THBUB mkafanye majukumu yenu kama mlivyopangiwa na mkawe tayari kupokea kauli zote za wananchi." Amesema Mhe. Mwaimu.
Maafisa hao wamepangiwa kazi katika Ofisi za THBUB zilizopo Dodoma, Mtwara na Mwanza.