emblem

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu

Habari

WATUMISHI TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA WASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEI MOSI.


Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora(THBUB)wameungana na Wafanyakazi wengine nchini katika kuadhimisha maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi.

Maadhimisho hayo kitaifa yalifanyika Jijini Dodoma,Katika viwanja vya Jamhuri na mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu Hassani.

Pamoja na kushiriki katika maadhiisho ya Mei mosi kitaifa pia Watumishi wa THBUB Ofisi za Matawi wameshiriki maadhimisho hayo katika Mikoa ambayo Ofisi za Tume zinapatikana nchini.

Kauli mbiu ya Mwakaya sherehe za Wafanyakazi 2022 ni ‘’Mishahara na Maslahi bora kwa wafanyakazi ndio kilio chetu;Kazi iendelee.