ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Balozi Pindi Chana ateta na Mwenyekiti wa Tume

23 Oct, 2023
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Balozi Pindi Chana ateta na Mwenyekiti wa Tume

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.Balozi Dkt.  Pindi Chana amekutana na kufanya mazungumzo  na Mwenyekiti  wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu,  Mhe. Mathew  Mwaimu.

Mazungumzo yao yamefanyika leo tarehe  21 Oktoba, 2023 pembezoni mwa Kikao cha 77 cha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kinachoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha.

Wakati huohuo,  Mhe.Balozi Chana amekutana na kufanya mazungumzo  na Viongozi wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ambao ni Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu Bw. Frank Kanyusi na Naibu Kabidhi Wasii,  Bi.Irene Lesulie.