ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Kongamano la Kukuza Maadili na Mapambano Dhidi ya Rushwa

30 Nov, 2022

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kushirikiana na TAKUKURU inatarajia kuandaa kongamano la wanafunzi wanachama wa Klabu za Wapinga Rushwa na Kaki za Binadamu na Utawala Bora kutoka vyuo vya Kati na Vyuo vya Elimu ya Juu vilivyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma tarehe 26 Novemba, 2022. Kongamano hilo linatarajia kufanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma kuvihusisha vyuo mbalimbali vilivyopo Jijini Dodoma. Mgeni Rasmi katika Kongamano hilo ni Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb), Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Katika kongamano hilo, mada mbalimbali zitawasilishwa na kujadiliwa na washiriki hususan wanafunzi na wadau wengine kutoka taasisi za serikali. Mada kuu itakuwa ni “Kukuza Maadili na Mapambano Dhidi ya RushwaKuzuia Rushwa ni Jukumu Lako na Langu Tutimize Wajibu Wetu. Watoa Mada watakuwa ni Profesa Lugano Kusiluka Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Ndugu P. K. Ntwina, Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Dkt. Ombeni Msuya, Mwenyekiti Kamati ya Maadili kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, Naibu Makamu Mkuu, Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu na Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma TAKUKURU. 

 

Vyuo vinavyotarajiwa kushiriki ni Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini, Chuo cha Serikali za Mitaaa Hombolo, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Chuo cha Mtakatifu Johns’. Kongamano hilo linatarajia kufanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Kongamano hilo linatarajia kuja na mikakati ya kuhamasisha na kuhakikisha vijana kushiriki katika Kulinda, Kukuza na Kuhifadhi Haki za Binadamu, Utawala Bora, Maadili na Mapambano Dhidi ya Rushwa Nchini.

Katika Kongamano hilo wanafunzi pamoja na watumishi wa Chuo Kikuu cha Dodoma watapata fursa ya kuchangia mada kwa kutoa maoni, mapendendekezo na kuuliza maswali kukuhusu agenda itakayowasilishwa.