ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

SIKU YA MAADILI NA HAKI ZA BINADAMU, TAREHE 10 DESEMBA, 2022

21 Nov, 2022

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) itaungana na Wadau wa Kitaifa na Jumuiya ya Kimataifa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu.

Siku ya Haki za Binadamu huadhimishwa kila mwaka kama kumbukumbu ya kupitishwa Tamko la Dunia la Haki za Binadamu la mwaka 1948.

Siku hiyo pia itakuwa Siku ya Kiatiafa ya Maadili na Haki za Binadamu.

Siku ya kilele cha Maadhimisho, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Prof. Dkt. Ibrahim Juma, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania

Kauli Mbiu ya Maadhimiasho ni:

Maadili, Haki za Binadamu, Utawala Bora na Mapambano Dhidi ya Rushwa ni Jukumu la Pamoja Kati ya Serikali, Wananchi na Wadau Wengine’.

Taasisi nyingine zitakazoshiriki katika maadhimisho haya kwa kutoa huduma kwa wananchi katika eneo la Viwanja vya Nyerere squire Jijini Dodoma kuanzia tarehe 6 Disemba, 2022.ni:-

  • NIDA
  •  RITA
  • Jeshi la Polisi Tanzania
  •  Chama cha Wanasheria Tanganyika
  •  Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA)
  •  Ofisi ya Taifa ya Mashtaka
  •  Chama cha Mawakili wa Kujitegemea Tanganyika (TLS)  na
  • AZAKI zinazotoa msaada wa Kisheria kama vile Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).