ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Tume, TAKUKURU na LHRC washirikiana kutoa Elimu juu ya Haki za Binadamu, Utawala bora na Mapambano dhidi ya Rushwa.

30 Nov, 2022

Tarehe 01 Disemba, 2022 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)  pamoja na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) inatarajia kutoa elimu kuhusu Haki za Binadamu, Utawala Bora na Mapambano Dhidi ya Rushwa katika Soko la Chang'ombe na Chamwino yaliyopo katika Jiji la Dodoma.

Program hii ni sehemu ya Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto pamoja na Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu ambapo kilele chake kitakuwa tarehe 10 Disemba, 2022.