emblem

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu

Habari

kikao cha kupokea Mrejesho wa Mfumo wa Kujitegemea wa Malalamiko kutoka WDL na Synergy


Julai 21,2022 Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe.Mohamed Hamis Hamad amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Kampuni yaWILLIAMSON DIAMOND LTD(WDL),Katika Ofisi za Tume zilizopo Mtaa wa Kilimani Jijini Dodoma.

Lengo la mazungumzo hayo ilikuwa kuwasilisha mrejesho wa Mfumo wa kujitegeme wa Malalamiko(Independent Grievance Mechanism) ambao si wa kimahakama unaoratibiwana kampuni yaSynergy,ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kanuni za Mwongozo wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu na Biashara.

Aidha dhumuni la kuanzisha mfumo huo nikusaidia Kampuni ya mgodi ya WDL katika kutatua migogoro na Malalamiko ya Wananchi yaliyosababishwana Kampuni ya Ulinzi ya WDL Mwaka 2009. mfumo huo wa Synergy unatarajia kuimarishamahusiano kati ya WDL na Wananchi wa Vijiji kumi na mbili katika Wilaya ya Kishapu vinavyozunguka Mgodi huo.

Awali ujumbe wa kampuni ya WDL na Synergy ilitembelea Taasisi mbalimbali ikiwemoTume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kukusanya maoni ya namna nzuri ya kuanzisha mfumo wa kujitegemea wa kushughulikia malalamiko ili kusaidia jamii inayouzungukwa na maeneo hayo ya mgodi ili kupata nafuu ya madhara waliyoyapata kutokana na utendajikazi wa kampuni ya ulinzi iliyokuwa ikilinda eneo la Mgodi wa WLD .

Kikao hicho kilihudhuriwa na Mhe.Mohamed HamisHamad Makamu Mwenyekiti, Kamishna Mhe.Dkt. Thomas Masanja , Bwa. Patience Ntwina Katibu Mtendaji , Bi.Jovina MuchunguziAfisa Mchunguzi Mkuu(anayeshughulikia Haki za Binadamu na Biashara) , Bwa.Chrisantus Ndibaiukao Afisa Mchunguzi Mkuu (anayeshughulikia Haki za Binadamu na Biashara) wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Kwa upande wa Wageni ni Bwa.Ayoub MwendaMkurugenzi Mkuu (WDL),Paul Kupelus Mkurugenzi(Synergy),Sylivia Mulogo Mwanasheria(WDL),Bahame Nyanduga Mshauri(Synergy) Bernard Mihayo Meneja wa Maendeleo ya Jamii(WDL).