ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Wapatiwa Elimu ya Tume na Haki za Binadamu

14 Aug, 2026
Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Wapatiwa Elimu ya Tume na Haki za Binadamu

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), kupitia Tawi la Mtwara, imeendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya wananchi wanaotembelea banda lake katika Maonesho ya Nanenane 2026 yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi.

Leo Agosti 03, 2026 , mMdiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi wamepatiwa elimu kuhusu majukumu ya THBUB pamoja na umuhimu wa kulinda, kuheshimu na kuendeleza haki za binadamu katika utekelezaji wa majukumu yao ya uongozi.

Akitoa elimu hiyo, Afisa Mfawidhi THBUB Tawi la Mtwara Bw. Juma Mleli amesema viongozi wa Serikali za Mitaa wana nafasi muhimu katika kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa kwa kuzingatia sheria, usawa, uwajibikaji na utawala bora wakati wa kuwahudumia wananchi.

Aidha, Bw. Mleli amebainisha kuwa Tume itaendelea kushirikiana na viongozi wa ngazi mbalimbali katika kutoa elimu kwa umma ili kuongeza uelewa kuhusu haki za binadamu na kuimarisha utawala bora nchini.

Pia amewataka madiwani kutumia nafasi zao za uongozi kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuheshimu na kulinda haki za binadamu, akisisitiza kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu na kuimarisha amani, mshikamano na maendeleo ya jamii.

Kwa upande wao, madiwani wamei shukuru Tume kwa elimu waliyoipata, wakieleza kuwa elimu hiyo imewaongezea uelewa kuhusu majukumu ya Tume na kuwajengea uwezo wa kuhamasisha wananchi juu ya masuala ya haki za binadamu na utawala bora katika maeneo yao.

THBUB inaendelea kutumia Maonesho ya Nanenane 2026 kama jukwaa la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu haki za binadamu na utawala bora, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa jukumu lake la kuhamasisha jamii kutambua, kuheshimu na kulinda haki za binadamu nchini.

slot gacor