Idara ya Elimu kwa Umma, utafiti na Nyaraka
Majukumu ya Divisheni
i.Kuishauri Tume kuhusu masuala ya elimu kwa umma na mawasiliano;
ii. Kuandaa na kusambaza machapisho ya elimu kuhusu haki za binadamu, wajibu wa raia na huduma zitolewazo na Tume;
iii. Kufanya tafiti kuhusu hali ya haki zabinadamu na utawala bora nchini;
iv. Kusimamia Kituo cha Haki za Binadamu na Utawala Bora cha Nyaraka na Taarifa;
v. Kufanya uchambuzi na tathmini ya kimfumo kuhusu masuala ya haki za binadamu na utawala bora;
vi. Kuandaa miongozo ya utekelezaji wa majukumu ya Idara; na
vii. Kuandaa taarifa za kila mwaka, za vipindi maalum na za dharura kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Tume pamoja na hali ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

