ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Serikali yadhamiria kuboresha upatikanaji wa Haki Nchi.

27 Sep, 2022
Serikali yadhamiria kuboresha upatikanaji wa Haki Nchi.

 

Serikali  imedhamiria kutatua changamoto zinazotokana na ukosefu  wa haki  za Wananchi kwa kuekeza kwenye miundombinu ,rasilimali watu na fedha katika  taasisi zinazojihusisha na kutoa haki pamoja  na misaada ya kisheria ili kuhakikisha wananchi wanafakiwa kwa wakati  na kupatiwa huduma hizo.

Taasisi mbalimbali zinazohusika na masuala ya  Haki za Binadamu na Utawala Bora  zimejitokeza kushiriki shamrashamra za maadhimisho ya Miaka 20  ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ambapo taasisi hizo hufanya kazi kwa kushirikiana na tume katika kuhudumia  jamii.

Akiongea na waandishi wa Habari,Katibu Tawala Mkoa  wa Dodoma,Dkt.Fatma Mganga alipotembelea washiriki wote katika maonesho hayo,amejifunza mambo mengi na amejionea jinsi ambavyo Serikali imewekeza vya kutosha katika kuhakikisha huduma za kisheria na haki zinapatikana  kwa mwananchi wa chini bila gharama yoyote.

“Tumemsikia Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan mara nyingi akisisitiza kwamba  vyombo vinavyoshughulika  na masuala ya haki na utawala bora,itoshe tu kusema serikali imefanya uwekezaji mkubwa kuhakikisha  huduma ya haki na misaada ya kisheria inawafikia wananchi wote hasa wa ngazi ya chini”alisema Dkt. Fatma

Aliongeza kwamba hivi sasa jamii inakabiliwa na changamoto ya mmomonyoka wa maadili kuanzia ngazi ya familia jambo linalo pelekea ongezeko la matukio yasiyo na maadili hivyo kuongeza uhitaji wa taasisi zinazotoa misaada ya kisheria katika kutoa haki za binadamu na utawala bora kwa ujumla.

“Nimepita katika banda linaloshuguhulika na maadili kwa viongozi,nimeona ni jambo jema lakini nitoe rai kwa Watanzania wenzangu hasa wazazi kuijenga maadili kwa viongozi wetu,ni lazima tuanze kuwajenga watoto wetu,ukimkuza mtoto mwenye maadili tutapunguza matatizo mengi ambayo jamii inakabiliana nayo ikiwemo mauaji,rushwa,dhuruma na hivyo tutatengeneza jamii yenye kuzingatia maadili,haki na utawala bora,”alisema  Dkt. Fatma