emblem

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu

Habari

THBUB YAPONGEZWA KWA KUWEKA MKAKATI KUTENGENEZA MPANGO KAZI WA HAKI ZA BINADAMU NA BIASHARA NCHINI.


Waziri wa Katiba na Sheria. Dkt. Damas Ndumbaro(MB) ameipongeza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kuona umuhimu wa kutengeneza mpango kazi wa Haki za Binadamu na nchini.

Mhe. Ndumbaro alitoa pongezi hizo Aprili 22,2022 wakati wa kikao kazi cha kuitambulisha Tume na majukumu yake katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Katiba na Sheria uliopo Mji mkuu wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

“Niwapongeze kwa andiko hilo,naimani andiko hilo litatibu matatizo ya haki na biashara nchini kwa kizazi cha sasa na baadae ’’Alisema Mhe. Ndumbaro

Aidha Mhe.Ndumbaro alitoa wito kwa Tume kuendelea na mchakato huo wa andiko kwa kushirikiana na wadau wengine ili kuhakikisha kuwa tunasheria ya haki na usawa itakayosimamia haki za biashara nchini.

Awali akiwasilisha rasmi tamko kwa serikali Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe.Mathew P.M.Mwaimu (JajiMstaafu) alisema kuwa mkakati wa kutengeneza mpango kazi wa haki za binadamu na biashara utasaidia kuepushaa migogoro hasa ya ardhi hasa kwa upande wa fidia inapotokea kuanzishwa kwa shughuli za biashara.

Mhe. Mwaimu alieleza kuwa ,Tume Katika kutekeleza masuala ya Haki za Binadamu na Biashara, inafanya uchunguzi, ufuatiliaji, tathimini, utafiti, kuendesha midahalo na kutoe elimu kwa wadua wa haki za binadamu na biashara pamoja na umma.

‘Tume kupitia kazi hizo imebaini kuwa shughuli za biashara kupitia sekta mbalimbali hupelekea uvunjifu wa haki za binadamu.’Alisema Mhe Mwaimu

Kwa hatua ingine Mhe.Ndumbaro alitoa rai kwa Tume kuweka utaratibu mzuri wa kushirikiana na Taasisi binafsi zinazoshughulikia maswala ya haki za binadamu na utawala bora nchini ili kuwa na taarifa za pamoja,Ikiwa pamoja na kuandaa andiko la haki jinai nchini