ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Mineral Resources Institute - MRI.

30 Nov, 2022

Tume inatarajia kutembelea chuo hiki tarehe 03 Disemba, 2022 kwa lengo la kutoa elimu kuhusu THBUB, Haki za Binadamu, Utawala Bora, kuanzisha Vilabu vya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Utaratibu wa Kuanzisha Vilabu vya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika taasisi za elimu, Rushwa na Maadili, Kampeni ya Kimataifa ya Siku 16 ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto, Maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu na Maadili Duniani. Katika programu hii takriban watu 300 wanatarajia kufikiwa wakiwemo walimu, wafanyakazi na wanafunzi. Programu hii itakiwezesha chuo hiko kuanzisha Klabu ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, kuhamasisha na kuamsha uelewa juu ya masuala mbalimbali yanayohusiana na haki za binadamu na misingi ya utawala bora hususan katika sekta ya Madini na Biashara, kuitangaza THBUB, kuimarisha mashirikiano baina ya THBUB na Taasisi hiyo.