ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Hakisports washiriki Ufunguzi wa SHIMIWI Iringa

05 Oct, 2023
Hakisports washiriki  Ufunguzi wa SHIMIWI Iringa

Oktoba 4,2023 Wanamimchezo wa Hakisports wameshiriki  ufunguzi wa Mashindano ya Shirikisho la Michezo  la Wizara na  Idara za Serikali(SHIMIWI) yaliyofanyika Viwanja vya Samora,Mkoani Iringa.

Mgeni rasmi wa ufunguzi wa Mashindano hayo  ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri Nishati Mhe. Dkt.Doto Biteko Kwa Niaba ya Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania  Mhe.Samia Suluhu Hassan.

Aidha Mhe. Dkt Biteko amewahimiza Watanzania ikiwemo wanamichezo wanaoshiriki mashindan ya 37 ya  Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali(SHIMIWI) kuhakikisha kuwa  na mpango maalum wa kuendelea na  michezo mahali pa kazi ili iwe  tija na uwajibika kwa wafanyakazi.

Mhe Dkt Biteko ametoa wito  kwa waajiri  kutoa fursa kwa wafanyakazi kushiriki mashindano hayo kwani yana lengo la kuwakutanisha Watumishi mbalimbali kutoka Wizara na taasisi za Serikali kufahamiana.

“Nawaasa sana wafanyakazi kujituma kwa bidii na kushiriki michezo ili kujiepusha na maradhi pamoja na kuweka mashirikiano baina ya Wizara na taasisi kpiti mashindano hayo”.

 Kwa upande wake  Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw.Patience Ntwina amewapongeza wanamichezo wa Hakisports kwa kufanya vizuri  katika michezo iliyopita

“Naamini kupitia michezo hiyo mtajipanga vyema katika mashindano yajayo”alisema Bw.Ntwina

Mashindano ya Shirikisho la Michezo  la Wizara na Idara za Serikali(SHIMIWI) yalianza tarehe 27 Septemba,2023 Mkoani na kutarajia kumalizikia  Oktoba14,2023.