ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

WATUMISHI WA THBUB WAPATIWA MAFUNZO YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI

30 Mar, 2026
WATUMISHI WA THBUB WAPATIWA MAFUNZO YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI

Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) wamepatiwa mafunzo kuhusu masuala ya fidia kwa wafanyakazi, yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), kwa lengo la kuwaongezea uelewa katika kushughulikia malalamiko yanayohusu fidia kwa wafanyakazi.

Mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika Machi 25 na 26, 2026, katika jengo la Kambarage ambako kuna ofisi za WCF, na yamehusisha watumishi kutoka idara zote za Tume hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mtendaji, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw. Jackson Nyamwihula, amesema mafunzo hayo ni muhimu katika kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya msingi ya THBUB, hususani katika kulinda na kuendeleza haki za binadamu pamoja na misingi ya utawala bora.

Aidha, ameongeza kuwa THBUB itaendeleza ushirikiano wake na WCF ili kuhakikisha wafanyakazi wanapata haki zao za msingi kwa mujibu wa sheria.

Kwa ujumla, mafunzo haya yanatarajiwa kuongeza ufanisi wa watumishi wa THBUB katika kushughulikia malalamiko ya wafanyakazi kwa weledi zaidi, na hivyo kuchangia kuimarika kwa haki na ustawi wa wafanyakazi nchini.