ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YAKABIDHIWA VITENDEA KAZI VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 956.8

16 Apr, 2026
THBUB YAKABIDHIWA VITENDEA KAZI VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 956.8

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt Juma Zuberi Homera (Mb) amekabidhi vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi milioni 956.8 kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa lengo la kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya tume hiyo katika kulinda na kuhifadhi haki za binadamu na misingi ya utawala bora nchini.

Vitendea kazi hivyo ambavyo ni magari matano na kompyuta mpakato 30 vimekabidhiwa Aprili 15, 2026   wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Ofisi za Wizara hiyo, Mtumba Jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mhe. Dkt. Homera amesema kuwa Serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeweka kipaumbele katika kuboresha mazingira ya utendaji kazi na kuhimiza kutumia fursa iliyopo ya maendeleo ya TEHAMA nchini katika kuimarisha mifumo ya utoaji huduma kwa umma kwa njia za elektroniki.

…hivyo kwa upande wa Sekta ya Sheria, matumizi ya TEHAMA siyo hiari tena, bali ni hitaji la msingi katika kujenga mfumo wa haki unaokwenda sambamba na mahitaji ya karne hii amesema Mhe. Dkt. Homera.

 Aidha, Mhe. Homera amesema kuwa Wizara kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) imeona ni vyema kuziwezesha taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kwa kuzipatia vitendea kazi ili kuimarisha uwezo wa taasisi katika kuwahudumia Watanzania.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bw. Patience Ntwina akitoa shukurani baada ya kupokea vitendea kazi hivyo, amewashukuru sana Waziri wa Katiba na Sheria, Bw. Juma Zuberi Homera na Katibu Mkuu, Bw. Eliakimu Maswi kwa kuwezesha THBUB kupata vitendea kazi hivyo ambapo vitapunguza changamoto katika utendaji kazi.

"Vitendea kazi hivi vitaongeza tija na ari ya watumishi katika utekelezaji wa majukumu ya THBUB katika kuwahudumia wananchi, tunashukuru sana" amesema Bw. Ntwina.