KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
                            
                                 04 Mar, 2025
                            
                                
                             
                                Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2025, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeendelea kutoa elimu ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora mkoani Arusha katika Viwanja vya TBA vilivyopo Mtaa wa Kaloleni, Kata ya Mianzini.
Wananchi mbali mbali wamejitokeza katika Banda la THBUB kupata huduma ya ushauri wa kisheria, elimu kuhusu haki za binadamu na misingi ya utawala bora katika viwanja hivyo.

