ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YAPOKEA NA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO MBALIMBALI KATIKA MAONESHO YA UTUMISHI WA UMMA

19 Jun, 2026
THBUB YAPOKEA NA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO MBALIMBALI KATIKA MAONESHO YA UTUMISHI WA UMMA

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu haki za binadamu na utawala bora sambamba na kupokea na kushughulikia malalamiko mbalimbali katika Maonesho ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma leo Juni 18, 2026.

Akiongoza utoaji wa elimu hiyo, Kaimu Katibu Mtendaji wa THBUB ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Binadamu na utawala bora , Bi. Suzan P. Ndeona amefafanua kuhusu msingi wa kuanzishwa kwa Tume kwa mujibu wa Katiba, majukumu yake, pamoja na huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wananchi.

Amesema Tume inaendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo wanafunzi kupitia uanzishwaji wa vilabu vya haki za binadamu katika taasisi za elimu.

Akizungumzia mwitikio wa wananchi, Mchunguzi Mkuu Msaidizi wa THBUB, Bw. Botea Halfani amesema zaidi ya wananchi 35 wametembelea banda la Tume kupata elimu na kuwasilisha changamoto mbalimbali zinazowakabili ili zipatiwe ufumbuzi.

Amesema baadhi ya malalamiko yaliyopokelewa yanahusu mtoto kukosa matunzo kutoka kwa wazazi wake pamoja na mgogoro wa ardhi uliowasilishwa na mwananchi kutoka mkoani Manyara. Malalamiko hayo yamefanyiwa kazi na wahusika kuelekezwa katika mamlaka husika kwa hatua zaidi za utatuzi.

THBUB inaendelea kutumia maonesho hayo kama jukwaa la kuwafikia wananchi kwa karibu, kuwajengea uelewa kuhusu haki zao na kusikiliza changamoto zinazohusu haki za binadamu na utawala bora. Wananchi wote wanakaribishwa kutembelea banda la Tume ili kupata elimu, ushauri na huduma mbalimbali zinazotolewa.

slot gacor