ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

TUME YA HAKI ZA BINADAMU YAIMARISHA ELIMU NA UFUATILIAJI HAKI MAGEREZANI NA MASHULENI.

03 Jul, 2026
TUME YA HAKI ZA BINADAMU YAIMARISHA ELIMU NA UFUATILIAJI HAKI MAGEREZANI NA MASHULENI.

Katika jitahada za kuhakikisha haki na usawa vinapatikana kwa kila Mtanzania, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imeendelea kutekeleza jukumu lake la kutoa elimu ya haki za binadamu kwa makundi wakiwemo wanafunzi wa vyuo na shule za sekondari na msingi pamoja na kufanya ukaguzi wa magereza na sehemu wanamozuiliwa watu kwa mujibu wa sheria.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Zanzibar, Bw. Juma Msafiri Karibona alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Julai 2, 2026 katika banda la Tume wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa, Sabasaba.

Bw. Karibona ameeleza kuwa mojawapo ya jukumu la kikatiba la tume hiyo ni kuwawezesha wananchi kufahamu haki zao za msingi, sambamba na kuhakikisha mifumo ya kisheria inaheshimiwa katika ngazi zote.

"Tunaendelea kujikita katika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu haki za binadamu. Vile vile tunafuatilia kwa karibu masuala ya haki za binadamu ili kuhakikisha sheria za nchi zinafuatwa na kuweka mkazo katika kudumisha amani na utawala bora nchini,” alisema Bw. Karibona.

Akizungumzia utaratibu wa kupokea malalamiko ya uvunjifu wa haki za binadamu, Naibu Katibu Mtendaji huyo amebainisha kuwa tume ina wajibu wa kupokea na kuchunguza malalamiko kutoka kwa wananchi au makundi mbalimbali yanayodai kuvunjiwa haki zao.

"Tunapokea na kuyafanyia kazi malalamiko ya wananchi ambao wanahisi haki zao zimekiukwa kwa namna yoyote ile. Lengo letu ni kuhakikisha kila raia anapata haki na utawala bora bila ubaguzi,” alifafanua Bw. Karibona.

Ameongeza kuwa utekelezaji wa majukumu hayo unategemea misingi ya mikataba ya kimataifa na kikanda ambayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeiridhia.

Katika hatua nyingine, Bw. Karibona amesema tume hiyo inafanya utafiti wa kina katika maeneo yenye changamoto, hususan migogoro ya ardhi, ili kubaini vyanzo vyake na kupendekeza mikakati ya kutatua migogoro hiyo kwa misingi ya haki na sheria.

slot gacor