MAY DAY ZANZIBAR
Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ofisi ya Zanzibar, wameshiriki kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani (MAY DAY).
Kilele cha maadhimisho hayo kilifanyika viwanja vya Nanenane vilivyopo Dole, Kizimbani Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 01 Mei, 2026 huku mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi.
Awali shamra shamra za May Day zilitanguliwa na Maonesho ya "May day" yaliyozinduliwa Aprili 27, 2026 na Waziri wa Kazi na Uwekezaji, Mhe. Sharif Ali Sharif ambayo yataendelea hadi May 04, 2026.
Kauli mbiu ya mwaka huu kilele cha siku ya wafanyakazi ni "Upatikanaji wa Haki na Mazingira Bora Kazini, ni Msingi wa Uwajibikaji, Nidhamu na Maadili ya Wafanyakazi".

