ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

MTUMISHI AJIRA MPYA AAPISHWA KUWA MTUMISHI WA THBUB

28 May, 2025
MTUMISHI AJIRA MPYA AAPISHWA KUWA MTUMISHI WA THBUB

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Dkt. Thomas Masanja, amemuapisha Mtumishi Mpya Bw. Bryan B. Kimario kuwa Mtumishi wa THBUB katika kada ya Uhasibu Daraja II. 

Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za THBUB Makao Makuu, Mtaa wa Kilimani, Dodoma, Mei 27, 2025.

Wakati wa uapisho huo, Kamishna Dkt. Masanja amesisitiza umuhimu wa kuzingatia taratibu za kazi, akimhimiza Kimario kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu, ufanisi na kujituma, kwa manufaa ya taasisi na jamii kwa ujumla.