ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu ashiriki Kongamano la kujadili sensa ya watu na makazi kwa muktadha wa haki za Watu wenye Ualbino.

20 Jun, 2023
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu ashiriki Kongamano la kujadili sensa ya watu na makazi kwa muktadha wa haki za Watu wenye Ualbino.

Juni 12,2023 Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Mhe.Mathew Mwaimu ameshiriki katika Kongamano la kujadili sensa ya watu na makazi kwa muktadha wa haki za Watu wenye Ualbino.

Kongamano hilo lililofanyika ukumbi wa Misheni,Bombambili,mjini Songea lilifunguliwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt.Louis Chomboka kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma na kuhudhuriwa na Wanachama wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania pamoja na wadau mbalimbali.

Katika Kongamano hilo mada kuu nne(4)zilliwasilishwa na kujadiliwa.