ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YASHIRIKI KATIKA KIKAO KAZI CHA KUBORESHA MFUMO WA UTOAJI TAARIFA KWA TAASISI ZA HAKI JINAI NCHINI.

06 Jun, 2026
THBUB YASHIRIKI KATIKA KIKAO KAZI CHA KUBORESHA MFUMO WA UTOAJI TAARIFA KWA TAASISI ZA HAKI JINAI NCHINI.

Wizara ya Katiba na Sheria imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha utoaji wa haki nchini kupitia matumizi ya teknolojia ya kisasa kwa kukutanisha viongozi na wataalamu kutoka taasisi za haki jinai nchini kwa lengo la kujadili maendeleo ya mfumo wa National Legal Information System (NaLIS).

Katika kikao hicho Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) iliwakilishwa na Bw. Said Zuberi, Afisa Uchunguzi Mkuu kutoka Kitengo cha Taasisi za Haki Jinai.

Akifungua kikao hicho Juni 3, 2026 Mtumba Jijini Dodoma kwa niaba ya Katibu Mkuu Dkt. John Jingu, Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Sheria Bi. Jane Lymo alisema kuwa Wizara ya Katiba na Sheria ina jukumu la kiratibu, kusimamia na kufuatilia upatikanaji wa haki nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa wakati, usawa na ufanisi.

Akizungumza kwa niaba ya THBUB Bw. Said Zuberi alisema kuwa kuwepo kwa Mfumo wa Pamoja wa Utoaji Taarifa kutoka katika Taasisi za Haki Jinai nchini ni muhimu hususan katika kipindi hiki ambacho taasisi zinawasilisha taarifa za utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Kuangalia namna ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai Nchini.

Pia Bw. Said alisema kuwa ni muhimu mfumo ukaainisha aina ya taarifa zinazohitajika kwa kila taasisi kwani kila taasisi ina taarifa tofauti kulingana na mamlaka na majukumu yake. Aliongeza kuwa Mfumo huo utasaidia uwajibikaji katika utoaji wa taarifa.

Kikao hicho kimewakutanisha wadau mbalimbali wa mnyororo wa haki jinai ili kujadili aina ya taarifa zinazohitajika kuingizwa katika mfumo huo, namna bora ya kuzipata pamoja na mikakati ya pamoja yakuimarisha baina ya taasisi zinazohusika.

slot gacor