ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Simbachawene awataka wananchi kuitumia Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

08 Feb, 2022
Simbachawene awataka wananchi kuitumia Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.


Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. George Boniface Simbachawene amewataka Wananchi kuitumia Taasisi ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa kupeleka malalamiko yao badala ya kunung’unika na kufikia hatua ya kujinyonga kwa kuona wamekosa kusaidiwa.

Hayo amesema leoFebruari 7, 2022 baadaya kutembelea makao makuu ya ofisi ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Borazilizopo eneo la Kilimani jijini Dodoma na kuzungumza na Viongozi wa taasisi hiyo.

Mhe. Simbachawene amesema kuwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imeundwa kisheria, Wananchi waitumie taasisi hiyo ipasavyo ili kuweza kujua na kupata haki zao pale inapotokea haki zao zimevunjwa.

“Taasisi hii ina wataalam ambao kazi yao ni kusimamia haki za binadamu…, chombo hiki kina uwezo wa kufanya jukumu hilo kwa niaba ya mwananchi,” amesema Mhe. Simbachawene.

Aidha, Mhe. Simbachawene ametoa rai kwa Viongozi wa Serikali kuelekeza wananchi wenye matatizo na changamoto mbalimbali juu haki za binadamu na utawala bora kufika katika ofisi za Tume ili kuweza kupata ufumbuzi wa changamoto zao.

“Kuna baadhi ya majukumu yanaweza kusuluhishwa na ofisi za Mkuu wa Wilaya, mengine hawawez, chombo hiki kina watu ambao kazi yaokusuluhisha migogoro na kuweza kusajiliwa kwa utaratibu mzuri kabisa wa kudumu na ikawa imetatua tatizo,’’ amesema Mhe. Simbachawene.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Tume Mhe. Mathew Mwaimu amemshukuru Mhe. Simbachawene kwa kutembelea ofisi za Tume na kuongea na Uongozi.

“Kwa niaba ya viongozi wenzangu na watumishi wengine tunashukuru kwa ujio wako, na naamini mabadaliko makubwa yatatokea kupitia ujio wako – Asante Mhe. Waziri,” Mhe. Mwaimu amesema.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawaala bora ni idara huru ya Serikali,iliyoanzishwa kama taasisi ya kitaifa iliyo kitovu cha kukuza na kulinda haki za binadamu na utawala bora nchini Tanzania.THBUB ilianzishwa chini ya Ibara ya 129(1) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyorekebishwa na sheria Na.3 ya mwaka 2000.

Tume ilianza kazi Julai1,2001 baada ya kuanza kutumika kwa sheria ya Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora Sura ya 391 na Tangazo la Serikali Na.311la Juni 8,2001 na ilizinduliwa rasmi Machi15,2002 baada ya kuteuliwa na kuapishwa kwa Makamishna wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa upande wa Zanzibar, Tume ilianza kazi rasmi Aprili 30,2007 baada ya THBUB Sura ya 391 kuridhiwa na Baraza la Wawakilishi kwa kutungiwa sheria Na.12(Extension Act) ya Mwaka 2003.