ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YAFUATILIA MAJIBU YA MALALAMIKO YA WANANCHI KUHUSU UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU MBEYA

26 Nov, 2026
THBUB YAFUATILIA MAJIBU YA MALALAMIKO YA WANANCHI KUHUSU UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU MBEYA

 

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), kupitia Ofisi ya Tawi la Mbeya, imefanya ufuatiliaji wa majibu ya malalamiko ya wananchi kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu yaliyowasilishwa katika ofisi hiyo kutoka mikoa ya Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa na Rukwa.

Katika kutekeleza jukumu hilo, THBUB imetembelea Ofisi za Mashtaka na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Mbeya, kwa lengo la kufuatilia hatua zilizochukuliwa kuhusu malalamiko hayo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mfawidhi wa THBUB Tawi la Mbeya, Bi. Ritha Malisa, amesema ufuatiliaji huo ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya kisheria ya THBUB, ikiwemo kupokea, kufuatilia na kuchunguza malalamiko ya ukiukwaji wa haki za binadamu na kuhakikisha haki hizo zinaheshimiwa na kulindwa.

Bi. Ritha ameeleza kuwa THBUB inaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za umma na binafsi katika kushughulikia masuala ya haki za binadamu na utawala bora, ili kuhakikisha malalamiko yanayowasilishwa yanafanyiwa kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na misingi ya haki.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa taasisi za umma kushirikiana na THBUB kwa kutoa taarifa na kuwezesha upatikanaji wa nyaraka na taarifa muhimu zinazohitajika katika ufuatiliaji wa malalamiko, hatua inayochangia kuimarisha uwajibikaji na utawala bora.

Kupitia ufuatiliaji huo, THBUB inaendelea kusimamia utekelezaji wa majukumu yake ya kisheria kwa kuhakikisha malalamiko ya wananchi kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu yanafanyiwa kazi na misingi ya haki, usawa na uwajibikaji inazingatiwa katika utendaji wa taasisi za umma na binafsi.

slot gacor