ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YASHIRIKI KLINIKI YA SHERIA ARUSHA

26 Nov, 2026
THBUB YASHIRIKI KLINIKI YA SHERIA ARUSHA

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Wakili Dunford George Mpelumbe ameshiriki kupokea na kushugulikia malalamiko kuhusu masuala ya haki za binadamu kwa wananchi waliojitokeza kupata huduma ya ushauri katika Kliniki ya Sheria Bila Malipo iliyoandaliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika viwanja vya Sanawari Jijini Arusha.

Ushiriki huo umefanyika leo, Novemba 25, 2026, siku moja baada ya uzinduzi rasmi wa kliniki hiyo uliofanyika Novemba 24, 2026.

Akizungumzia ushiriki wa Tume katika kliniki hiyo, Mhe. Mpelumbe amesema ushiriki huo ni sehemu  ya mashirikiano katika ulinzi wa haki za binadamu na kutoa fursa kwa wananchi kupata haki zao kupitia msaada wa kisheria.

Ushiriki wa THBUB unaonesha dhamira ya Tume ya kuendelea kushirikiana na wadau katika kukuza, kulinda na kutetea haki za binadamu pamoja na kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wananchi.

slot gacor