ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini

i. Kuandaa na kutekeleza Mfumo Elekezi wa Ufuatiliaji na Tathmini (M&E) kwa ajili ya Tume;

ii. Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Muda wa Kati, mipango ya mwaka, bajeti, programu na miradi kwa kuzingatia Mfumo wa Mipango wa Kitaifa;

iii. Kufuatilia na kutathmini maeneo muhimu ya matokeo (Key Result Areas – KRA) ya Tume;

iv. Kufanya tathmini ya athari za mipango, programu na miradi inayotekelezwa chini ya Tume; 

 v. Kuandaa taarifa za Ufuatiliaji na Tathmini kuhusu Maeneo Muhimu ya Matokeo ya Kitaifa (NKRAs) yaliyo chini ya Tume;

vi .Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala na Maelekezo ya Serikali;

vii. Kuratibu Mfumo wa Taarifa wa Usimamizi wa Utendaji Kazi za Taasisi za Umma kupitia mfumo wa e-Utendaji (PEPMIS &PIPMIS);

viii.Kusimamia na kuhuisha kanzidata ya takwimu za Tume;

ix. Kuchambua taarifa za utendaji kazi za Tume za vipindi mbalimbali (kila wiki, kila mwezi, kila robo mwaka, nusu mwaka na mwaka) na kuandaa taarifa ya jumla ya utendaji kazi wa Tume; na

  x.  Kutoa msaada wa kitaalamu na kusimamia taratibu za Ufuatiliaji na Tathmini (M&E) ndani ya Tume.

 

 

slot gacor