ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI MEI MOSI, 2025.

14 May, 2025
THBUB YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI MEI MOSI, 2025.

Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Tawi la Dar es Salaam wameshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei mosi) ambayo kimkoa yamefanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe ,Wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo amewataka wafanyakazi kutambua wajibu wao na kwamba wao ndio taswira ya Serikali.

“Wafanyakazi tunaposherehekea siku hii tutambue kuwa sisi ndio tumebeba taswira ya Serikali kwani mfanyakazi mmoja anaweza kusababisha Serikali ichukiwe au ipendwe, hivyo wafanyakazi wote tuendee kufanya kazi kwa uaminifu na imani kwani Serikali inatujali na kutupenda” amesema Mhe. Chalamila 

Aidha, Mhe. Chalamila amewataka wafanyakazi wote kutekeleza kauli mbiu ya maadhimisho kwa kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu kwa kujiandikisha na kuchagua Madiwani, Wabunge pamoja na Rais.

Maadhimisho ya Mei Mosi 2025 yalikuwa na kauli mbiu isemayo “Uchaguzi Mkuu 2025, utuletee Viongozi wanaojali Haki na Maslahi ya Wafanyakazi, sote tushiriki”