ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YAWAHIMIZA WATUMISHI WAPYA KUZINGATIA MISINGI YA TUME HIYO.

14 Jul, 2025
THBUB YAWAHIMIZA WATUMISHI WAPYA KUZINGATIA MISINGI YA TUME HIYO.

 

KAMISHNA wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ofisi ya Zanzibar, Mhe. Khatibu Mwinyichande amewanasihi watumishi wa tume hiyo kufanyakazi kwa kuzingatia misingi ya kazi za tume kwa nidhamu, weledi na kufuata maadili ya kazi zao kwa mujibu wa taratibu, kanuni na Sheria za Utumishi wa Umma.

Kamishna Mwinyichande ametoa nasaha hizo kwenye ofisi za , tume hiyo, Mbweni Wiaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi, alipozungumza na watumzishi 10 waliohamia ofisini hapo kutoka taasisi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ)  ikiwa ni hatua za kuwakaribisha rasmi kwenye tume hiyo.

Akizungumza kuhusu kufanyakazi na THBUB Mhe. Mwinyichande amewasihi watumishi hao kufanya kazi zaidi kwa kuzingatia misingi mikuu inayoiongoza tume hiyo ambayo ni kuheshimu haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

“Kila mmoja ajue anafanyakazi kwa mujibu wa miongozo na maadili ya Tume, kazi za tume ni za kushirikiana ukiachia za kila mtu na kada ya utaalamu wake, ni vyema nyote mkaijua tume kwa undani wake ili iwe wepesi kwenu kuijua na kuinakili misingi ya kazi za tume muelewe haki inaanzia wapi na muweze kuifanyia kazi kwa kufuata misingi ya utawala bora.” alilisitiza Mhe. MwinyiChande.

 

Katika hatua nyengine, Mhe. Mwinyichande aliwawasisitiza watumishi hao kufanyakazi kwa timu ya kushirikiana ili kujijingea ufanisi na weledi wa kazi za tume sambamba na kuwanasisihi kuachana na mazoea waliyotokana nayo sehemu walizowahi kufanyia kazi hasa mazoea yenye kupotosha bali waboreshe na kujenga ustawi wa jamii iliyobora kwenye maeneo yao ya kazi.

Akizungumzia suala la utawala bora,  Kamishna Mwinyichande pia aliwasisitiza watumishi hao kulinyia kazi kwa uweledi na ufanisi wa hali ya juu eneo hilo ili kuhakikisha haki inatekelezwa kwa kila aliyefunjiwa.

Naye, Katibu Msaidizi wa THBUB, Juma Msafiri Karibona alikazia kwenye eneo la ushirikiano baina ya wafanyakazi hao wepya, waliohamia na wale wa zamani ili kujenga jamii iliyokusudiwa na tume hiyo kwa kuzingatia madili na sheria za Tume hiyo.

Kwa upande wa watumishi hao waliohamia kutoka kwenye taasisi za SMZ, waliiahidi tume kufanyakazi kwa ushirikiano wa hali ya juu ili kuifikisha Tume  pale inapostahiki kuwa.

Pia walieleza furaha yao ya kuendeleza utumishi wao kwa weledi na ufanisi wa hali ya juu kwa kufuata taratibu, kanuni na Sheria za utumishi wa umma.