TIMU YA HAKI KAMBA YAIBUKA NA USHINDI.

Timu ya Wanaume ya kuvuta Kamba ya Haki Sports imeibuka na Ushindi dhidi ya RAS Pwani katika Michuano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI). Mchezo huo ulichezwa katika Viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza mapema leo Septemba 1, 2025.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Kapteni wa Timu ya Kamba Bw. Kilua Mtae ameeleza kuwa, Timu hiyo imejipanga vizuri katika michezo yote iliyopangwa.
Aidha, Bw. Mtae amewapongeza wachezaji wote kwa kuwa makini pamoja na kuzingatia sheria zote zinazohusu mchezo huo wa kamba. "Hongereni sana" amesema
Katika Mchezo wa Kamba Wanaume Timu ya Haki imepangwa katika kundi H na kesho inatarajiwa kucheza na Maliasili.
Timu ya kuvuta Haki Sport ni miongoni mwa timu kutoka THBUB ambazo zinazoshiriki Michezo ya Kamba Michezo mingine ambayo THBUB inashiriki ni pamoja na Riadha